Ada Chuo Cha Usafirishaji NIT 2025/2026 Kozi za Diploma

Ada Chuo Cha Usafirishaji NIT 2025/2026 Kozi za Diploma

Chuo cha Usafirishaji cha NIT ni moja kati ya vyuo vilivyojizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na mchango wake mkubwa katika kutoa elimu ya juu bora katika nyanja za usafirishaji, uchukuzi, na usimamizi wa biashara za usafirishaji. Chuo hiki kimejikita katika kutoa mafunzo ya vitendo, utafiti, na ushauri wa kitaalamu katika sekta za usafirishaji wa anga, reli, barabara, maji, na bomba.

Kikiwa chini ya Wizara ya Uchukuzi, National Institute of Transport (NIT) ni taasisi ya umma ya elimu ya juu iliyoanzishwa kwa mujibu wa NIT Act Cap 187, ikiwa na dhamira ya kutoa elimu ya kitaalamu kwa kutumia mfumo wa Competence-Based Education and Training (CBET). Chuo kimeidhinishwa na NACTVET kufundisha ngazi za Cheti, Diploma, Shahada na Shahada ya Uzamili (NTA Level 4 – 9).

Kwa sasa NIT ina zaidi ya wanafunzi 16,000, vitivo vitano vikuu, na idadi kubwa ya wakufunzi wenye sifa za kitaaluma. Vitivo hivyo ni pamoja na:

  • Fakulti ya Usafiri wa Anga, Baharini na Teknolojia ya Petroli,
  • Fakulti ya Uhandisi wa Usafiri na Teknolojia,
  • Fakulti ya Usimamizi wa Usafirishaji na Biashara,
  • Fakulti ya Sayansi ya Habari na Mafunzo ya Kiufundi,

Pamoja na idara mbalimbali zinazotoa huduma za kitaaluma na maendeleo ya wanafunzi

Ada Chuo Cha Usafirishaji NIT 2025/2026 Kozi za Diploma

Ada Chuo Cha Usafirishaji NIT 2025/2026 Kozi za Diploma

Chuo cha Usafirishaji (NIT) kimeweka ada rasmi kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 kwa wanafunzi wa ngazi ya Ordinary Diploma (NTA Level 6). Ada hizi zinahusisha gharama za mafunzo, usajili, mitihani, chakula, malazi, na huduma nyingine muhimu za mwanafunzi.

Jedwali lifuatalo linaonesha ada za kila kozi ya Diploma kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 kulingana na taarifa rasmi ya NIT.

Kozi ya Diploma Ada kwa Mwaka (TZS) Muda wa Masomo
Diploma in Transport Management 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Logistics and Transport Management 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Procurement and Logistics Management 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Business Administration 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Human Resource Management 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Information Technology 1,350,000 Miaka 3
Diploma in Computing and Information Systems 1,350,000 Miaka 3
Diploma in Mechanical Engineering 1,400,000 Miaka 3
Diploma in Automobile Engineering 1,400,000 Miaka 3
Diploma in Civil Engineering 1,400,000 Miaka 3
Diploma in Electrical Engineering 1,400,000 Miaka 3
Diploma in Electronics and Telecommunication Engineering 1,400,000 Miaka 3
Diploma in Aircraft Maintenance Engineering 2,500,000 Miaka 3
Diploma in Freight Clearing and Forwarding 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Aviation Business Management 1,500,000 Miaka 3
Diploma in Road Transport Safety Management 1,250,000 Miaka 3
Diploma in Shipping and Port Management 1,500,000 Miaka 3
Diploma in Petroleum and Energy Management 1,600,000 Miaka 3
Diploma in Maritime Transport and Nautical Science 1,600,000 Miaka 3
Diploma in Transport Engineering 1,400,000 Miaka 3

Kwa taarifa zaidi kuhusu ada za kozi za diploma katika chuo cha NIT tafadhali angalia kupitia kiungo hiki > Taarifa zaidi juu ya Ada za NIT

Umuhimu wa Kuchagua NIT kwa wWanafunzi wa Diploma

NIT imejijengea sifa ya kuwa chuo kinachozalisha wataalamu wenye ujuzi wa vitendo unaohitajika katika sekta ya usafirishaji na teknolojia. Wanafunzi wa ngazi ya Diploma kutoka NIT hupata fursa ya kufanya mafunzo kwa vitendo (field practical training) katika mashirika ya kitaifa na kimataifa, sambamba na uwezekano wa kujiendeleza hadi ngazi ya Shahada ndani ya chuo hicho.

Kwa kuzingatia ubora wa walimu, mazingira rafiki ya kujifunzia, na programu za kisasa, NIT inabaki kuwa chaguo bora kwa wanafunzi wanaotaka taaluma ya usafirishaji, uchukuzi, teknolojia na biashara.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mwisho wa Kutuma Maombi ya Mkopo 2025/2026
  2. Ada Chuo Kikuu Cha Dar es salaam UDSM 2025/2026
  3. Kozi Zinazotolewa Chuo Cha Kairuki 2025/2026
  4. HESLB Yatangaza Kuongeza Muda wa Maombi ya Mikopo hadi 14/09/2025
  5. Orodha ya Vyuo Vikuu Tanzania Vilivyo Idhinishwa na TCU 2025/2025
  6. Vyuo vya Private Dar es Salaam 2025