Ada za Kozi ya Udereva NIT 2025 | Ada za Chuo cha NIT Driving Course 2025
Kozi za Udereva ni miongoni mwa kozi zilizojizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania kutokana na uhitaji mkubwa wa madereva stadi katika sekta mbalimbali. Kila siku makampuni na mashirika hutangaza nafasi za ajira kwa madereva wa mabasi, magari ya mizigo, magari ya kifahari (VIP), na hata vifaa vya viwandani kama Forklift. Wahitimu kutoka taasisi zinazotambulika kitaifa kama VETA na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) huwa na nafasi kubwa ya kunufaika na ajira hizo.
Kozi za Udereva zinazotolewa na NIT sio tu njia ya kupata leseni, bali ni fursa ya kupata mafunzo ya kina yanayowajengea madereva uwezo wa kuendesha kwa usalama, weledi, na kwa kufuata viwango vya kimataifa. Katika makala hii, tutaangazia ada za kozi ya udereva NIT kwa mwaka 2025, muda wa kozi, na masharti ya kujiunga.
Ada za Kozi za Udereva Zinazotolewa NIT 2025
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kupitia Idara ya Usalama Barabarani na Mazingira (Transport Safety and Environmental Engineering) hutoa aina mbalimbali za kozi fupi za udereva kila mwezi kutoka Januari hadi Juni 2025. Zifuatazo ni baadhi ya kozi kuu:

1. Passenger Service Vehicle (PSV) – Kozi ya Udereva wa Magari ya Abiria
- ️ Muda: Siku 11
- Ada: TSh 200,000/=
- Mahali: NIT – Dar es Salaam
- Masharti: Lazima ufanye na kufaulu jaribio la awali la vitendo (pre-test) kwa ada ya TSh 20,000/=
2. Heavy Goods Vehicle (HGV) – Kozi ya Udereva wa Magari ya Mizigo
- ️ Muda: Siku 15
- Ada: TSh 515,000/=
- Mahali: NIT – DSM
- NB: Kozi hii hufanyika kila mwezi kuanzia Januari hadi Juni
3. Advanced Driver Grade II (VIP) – Kozi ya Madereva wa VIP
- ️ Muda: Wiki 4
- Ada: TSh 400,000/=
- Mahali: NIT – DSM na pia inapatikana kituo cha Dodoma
- Pre-test ni sharti kwa wanaotaka kujiunga
4. Advanced Driver Grade I
- ️ Muda: Wiki 4
- Ada: TSh 420,000/=
- Mahali: NIT – DSM
5. Senior Driver (Assistant Fleet Manager)
- ️ Muda: Wiki 6
- Ada: TSh 450,000/=
- Mahali: NIT – DSM
- Inafaa kwa madereva wanaotaka kupanda daraja kuwa wasimamizi wa magari
6. Driver Instructor Course – Kozi kwa Walimu wa Udereva
- ️ Muda: Wiki 10
- Ada: TSh 600,000/=
- Mahali: NIT – DSM
- Sifa: Uzoefu wa udereva wa miaka 2 na leseni halali ya daraja husika
7. Forklift Operator’s Training – Kozi ya Uendeshaji Forklift
- ️ Muda: Siku 5
- Ada: TSh 400,000/=
- Mahali: NIT – DSM
Maelekezo Muhimu kwa Waombaji wa Kozi Za Udereva NIT 2025
- Pre-test ni lazima kwa kozi za PSV, HGV, na VIP. Ada yake ni TSh 20,000/=
- Malipo yote lazima yafanyike kwa namba ya malipo (control number) ya GePG kabla ya tarehe ya usajili
- Washiriki watajitegemea kwa malazi na chakula
- Kozi zitaanza pale tu idadi ya washiriki itakapokamilika
- Kozi zilizo na alama ya ** kama HGV au Forklift zitaanza iwapo idadi itatosha
- Wasiliana na NIT kabla ya malipo yoyote kwa uthibitisho
Mapendekezo ya Mhariri:
- Sifa za Kujiunga Kozi za Cheti (Certificate) Vyuo Mbalimbali
- Ada ya Chuo cha Mweka Fees 2025/2026
- Kozi Zinazotolewa Na Chuo Cha Wanyama Pori Mweka (CAWM) 2025/2026
- Sifa za Kujiunga na Chuo cha Wanyama Pori Mweka 2025/2026
- Orodha ya Vyuo Vya Utalii Tanzania 2025
- Vyuo Vya Hotel Management Tanzania 2025
- Sifa za Kujiunga Kozi za Stashahada (Diploma) Vyuo Mbalimbali









Leave a Reply