Nafasi Mpya Za Kazi MDAS Na LGAS 09-08-2025

Nafasi Mpya Za Kazi MDAS Na LGAS 09-08-2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs na LGAs), ametangaza nafasi mpya 199 za ajira katika nyanja mbalimbali kwa ajili ya watanzania wenye sifa stahiki.

Ajira hizi zinahusu kada tofauti zikiwemo elimu, kilimo, utamaduni, michezo, biashara, na uhandisi. Tangazo hili la nafasi za kazi linatoa fursa kwa wataalamu waliobobea katika taaluma mbalimbali kujiunga na utumishi wa umma, likiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa.

Orodha ya Nafasi za Kazi Zilizotangazwa

Kada Idadi ya Nafasi
Mhandisi Kilimo Daraja la II (Agricultural Engineer II) 5
Mwalimu Daraja la III C – Lishe (Food and Human Nutrition) 1
Afisa Hesabu Daraja la II (Accounts Officer II) 30
Mhifadhi Wanyamapori Daraja la II (Game Warden II) 35
Mwalimu Daraja la III B – Kemia (Chemistry) 30
Mwalimu Daraja la III B – Elimu Maalum 15
Mwalimu Daraja la III B – Fasihi ya Kiingereza (English Literature) 19
Mwalimu Daraja la III B – Uchumi (Economics) 2
Mwalimu Daraja la III B – Biashara (Commerce) 12
Afisa Maendeleo ya Michezo Msaidizi Daraja la II (Assistant Game and Sports Development Officer II) 18
Fundi Sanifu Daraja la II – Maji (Technician Grade II – Water) 1
Afisa Utamaduni Msaidizi (Assistant Cultural Officer II) 10
Fundi Sanifu Daraja la II – Umwagiliaji (Technician Grade II – Irrigation) 1
Opareta wa Kompyuta Msaidizi II (Assistant Computer Operator) 10
Afisa Biashara Msaidizi (Assistant Trade Officer) 40
Mpishi Daraja la Pili II (Cook II) 20

Nafasi Mpya Za Kazi MDAS Na LGAS 09-08-2025

Masharti ya Jumla kwa Waombaji

Wote wanaotarajia kuomba nafasi hizi wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:

Waombaji wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.

Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C lazima waambatishe hati ya matokeo (Academic Transcript) kwenye mfumo wa Ajira Portal kwa uthibitisho wa masomo ya kufundishia.

Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kutuma maombi na kueleza aina ya ulemavu katika mfumo wa maombi.

Kuambatanisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

Kuambatanisha wasifu binafsi (Detailed C.V) wenye anwani, namba za simu za kuaminika, na majina ya wadhamini watatu.

Kuambatanisha nakala za vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili kulingana na sifa za kazi husika, ikiwemo:

  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates
  • Cheti cha Kidato cha IV na VI
  • Vyeti vya Kompyuta
  • Vyeti vya kitaaluma kutoka bodi husika

Hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (Results Slips), Testimonials, Provisional Results au Statement of Results hazitakubaliwa.

Vyeti vilivyopatikana nje ya Tanzania viwe vimehakikiwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTE).

Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Waajiriwa walioko kwenye nafasi za kuingilia katika Utumishi wa Umma hawapaswi kuomba, isipokuwa kwa kuzingatia maelekezo ya waraka maalum wa Serikali.

Kuwasilisha taarifa au sifa za kughushi kutasababisha hatua kali za kisheria.

Mwisho wa Kutuma Maombi

Maombi yote yatatumwa kupitia mfumo wa Ajira Portal wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, na tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 22 Agosti 2025.

Tuma Maombi Sasa

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mfano wa Barua Ya Maombi ya Kazi ya Mwandishi Mwendesha Ofisi II
  2. Nafasi za Kazi ya Udereva Ajira Portal 2025
  3. Nafasi za Kazi ya Udereva Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni July 2025
  4. Nafasi Mpya Za Kazi Halmashauri Ya Mji Wa Mbulu 01-07-2025
  5. Nafasi Mpya za Kazi Amana Bank June 2025
  6. Nafasi Za Kazi Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika EASTC June 2025
  7. Nafasi Za Kazi Mamlaka Ya Usimamizi Wa Bandari Tanzania TPA June 2025