Ratiba ya Mtihani wa Taifa Kidato cha Pili 2025
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi ratiba ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (Form Two National Assessment – FTNA) kwa mwaka 2025, ambao utafanyika kuanzia Jumatatu, tarehe 3 Novemba hadi Alhamisi, tarehe 13 Novemba 2025.
Mtihani huu wa kitaifa ni wa aina ya tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi, ukiwa na lengo la kutoa mrejesho kwa walimu, wanafunzi na wadau wa elimu ili kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na NECTA, mitihani itafanyika kwa awamu mbili kila siku asubuhi kuanzia saa 2:00 hadi saa 4:30 asubuhi, na mchana kuanzia saa 8:00 hadi saa 10:30 alasiri kutegemeana na somo husika. Pia, baadhi ya mitihani ya vitendo na mipango ya mitihani maalum itaendeshwa hadi saa 7:00 mchana.
Muhtasari wa Ratiba ya Mtihani wa Taifa Kidato cha Pili 2025
- Tarehe ya Kuanza: Jumatatu, 3 Novemba 2025
- Tarehe ya Kumaliza: Alhamisi, 13 Novemba 2025
- Asasi Husika: Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
- Lengo: Kutoa tathmini ya kitaifa ya maendeleo ya kielimu kwa wanafunzi wa Kidato cha Pili nchini Tanzania
Ratiba ya Baadhi ya Masomo Muhimu:
| Tarehe | Asubuhi (8:00 – 10:30) | Mchana (2:00 – 4:30) |
| 3/11/2025 | Civics, Historia ya Tanzania (Vocational) | English Language (Regular & Vocational) |
| 4/11/2025 | Basic Mathematics, Math (Vocational) | Biology, Tourism (Vocational) |
| 5/11/2025 | Geography, Horticulture, Food Production | Kiswahili, Computer Application |
| 6/11/2025 | Chemistry, Life Skills (Vocational) | History, French, Arabic, Agriculture |
| 7/11/2025 | Physics, Engineering Science | Commerce, Electrical Engineering |
| 10/11/2025 | ICT, Computer Application (Practical) | Book-Keeping, Football Performance |
| 11/11/2025 | French, Additional Mathematics, Theatre | Bible Knowledge, Elimu ya Dini ya Kiislamu |
| 12/11/2025 | Fine Art, Agriculture, Civil Engineering | Music, Arabic, Woodwork |
| 13/11/2025 | Home Economics, Field Crop Production | Physical Education |

Pakua PDF Ya Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Pili 2025 Hapa
Maelekezo Muhimu kwa Wanafunzi
NECTA imeelekeza kuwa wanafunzi wote wanapaswa kuhudhuria mitihani kwenye vituo walivyoandikishwa rasmi. Aidha, mitihani itaendelea kufanyika hata ikiwa tarehe iliyopangwa ni siku ya sikukuu ya kitaifa.
Wanafunzi wanatakiwa:
- Kufika kwenye chumba cha mtihani kwa wakati (si zaidi ya dakika 30 baada ya mtihani kuanza).
- Kufuata maelekezo ya wasimamizi wa mtihani.
- Kutotumia vifaa au nyaraka zisizoruhusiwa.
- Kuandika kwa kalamu ya rangi ya buluu au nyeusi; michoro yote ifanyike kwa penseli isipokuwa ikielekezwa vinginevyo.
- Kuandika namba ya mtihani kwa usahihi katika kila ukurasa wa karatasi ya majibu.
Ukiukwaji wa maadili ya mtihani, ikiwa ni pamoja na udanganyifu, unaweza kusababisha mwanafunzi kufutiwa matokeo au kuzuiwa kushiriki mitihani ya baadaye.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mtihani wa Darasa la Nne 2025
- Tarehe Ya Kuripoti Shuleni Kidato cha Tano 2025
- Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 Yametangazwa Rasmi na NECTA: Ufaulu Waendelea Kupanda!
- Sheria Za Shule Za Sekondari Tanzania
- Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2025
- Kozi za Diploma Zenye Mkopo 2025/2026











Leave a Reply